PONGEZI ZA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN



Assalaamu alaykum warahmatullahi wabarakaatuh
Ukurasa wa MIMI NI MUISLAMU (Facebook) wakishirikiana na Blogi ya Dinullah tunakupeni pongezi kwa kujaaliwa kuufikia  mwezi mtukufu wa RAMADHANI. Mwezi wenye kheri na Baraka mbali mbali. Mwezi ambao ni jukumu la kila mmoja wetu kuufunga. Ni furaha iliyoje kuufikia mwezi huu!
Wangapi walitamani kufikishwa mwezi huu lakini hivi sasa hatupo nao tena Hatuna budi kumshukuru kwa dhati Allaah ‘azza wa jall kwa kutufikisha tena kwenye neema hii kubwa isiyo na mfano, Alhamdulillahi ewe Allah kwa kutufikisha tena katika mwezi huu mtukufu wa  Ramadhani.

Habibil Mustafa, Mtume Muhammad rehema na amani ziwe juu yake alikuwa  akiwapongeza na kuwabashiria kheri maswahaba wake kwa kujaaliwa kuufikia mwezi mtukufu wa RAMANDANI.
عَن أَبِي هُرَيْرَة رَضِي الْلَّه عَنْه قَال : قَال رَسُوْل الْلَّه صَلَّى الْلَّه عَلَيْه وَسَلَّم : " أَتَاكُم شَهْر رَمَضَان ، شَهْر مُبَارَك ، فَرَض الْلَّه عَلَيْكُم صِيَامَه ، تُفْتَح فِيْه أَبْوَاب الْجَنَّة ، وَتُغْلَق فِيْه أَبْوَاب الْجَحِيْم ، وَتُغَّل فِيْه مَرَدَة الْشَّيَاطِيْن ، وَفِيْه لَيْلَة هِي خَيْر مِن أَلْف شَهْر ، مَن حَرَّم خَيْرَهَا فَقَد حُرِم ".
(Umekujieni mwezi wa Ramadhani, mwezi wenye Baraka. Allaah kakufaradhishieni kufunga katika mwezi huu. Katika mwezi huu inafunguliwa milango ya mbinguni, na inafungwa milango ya motoni, na mashetani wanafungwa pia, katika mwezi huu kuna  usiku ambao ni bora kulikoni miezi alfu moja.Yule mwenye kuharamishiwa kheri zake hakika huyo kaharamishiwa kheri nyingi sana!)
Hivyo basi ni jukumu letu kufanya juhudi za hali ya juu ili kuhakikisha kwamba ni wenye kuzipata kheri za mwezi huu. Ewe Allah shukurani zote wastahiki wewe kwa kutufikisha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Ewe Allah tujaalie tuwe ni wenye kuupata usiku wa heshima (laylatu lkadr), usiku uliobora kuliko miezi elfu. Ewe Allah tuandikie malipo ya wenye kuudiriki usiku huo. Ewe Allah yakubali matendo yetu mema.
Allahuma aaaamiin