Mim Saakina

Maana ya  Mim Saakina (مْ)
Mim saakina (مْ) ni mim ambayo haina haraka na ina sukun isiyobadilika inaposomwa kwa kuendelea au kwa kusimama, yaani inapokuwa herufi ya mwisho kusomwa, kwenye hukmu za mim saakina (مْ) haingii mim (م) ambayo kwa asili haina haraka lakini imeingia haraka kutokana na herufi inayofuatia mbele yake. Lugha kiarabu hairuhusu herufi mbili zenye sukun kuwa pamoja kwa kufuatana, inapotokea makutano hayo, moja kati ya herufi mbili hizo huingia haraka.
Inapotokea herufi mbili zisizo haraka kuwa ni herufi madda yaani ا و ي (kwa ajili ya kuvuta), madda hufupishwa na hivyo kubakia herufi yenye haraka (katika kusoma na si katika kuandika)
Mim (م) inayokuwa mwisho wa neno ambayo ina haraka haingii katika hukumu za mimi sakina (مْ) japokuwa mim (م) hii hutamkwa bila ya haraka (kwa sukun), mim hii husomwa kwa sukun kwa vile husimamiwa. 
Mim sakina (مْ) inaweza kuwa katikati au mwisho wa neno, inaweza kuwa nomino (اِسْم) au kitenzi (فِعْل) Mim saakina  baadhi wa wakati na si mara zote huwakilisha wingi kwa mfano لَكُم na لَهُم 
Mim saakina ina hukmu tatu, nazo ni:-
الإِخْفَاء الشَّفّوِي
الإِدْغَام الصَّغِيْر
الإِظْهَار الشَّفّوِي