Ikhfaa Shafawi




Ikhfaa Shafawi (الإِخْفَاء الشَّفّوِي)
Maani yake: Ikhfaa katika lugha maana yake ni kuficha au kufunika na shafawi ni simulizi . Ikhfaa shafawi katika tajwid ni kutamka herufi isiyo na haraka  bila ya kutia shadda, baina ya kiwango cha idh-haar na idghaam, kwa makisio hutamkwa kiasi cha haraka mbili.
Herufi ya Ikhfaa shafawi: Ikhfaa shafawi ina herufi moja tu, nayo ni  baa (البَاء) 
Namna inavyotokea: Ikhfaa shafawi hutokea iwapo min saakina (مْ) itafuatiwa na baa (ب). Ikhfaa shafawi hutokea baina maneno mawili na hivyo meem saakina huwa mwisho wa neno la mwanzo na baa huwa ni herufi ya mwanzo katika neno la pili.
Namna inavyotamkwa: Meem hutamkwa kwa kufichwa na pia hutiwa ghunna, kutokana na kuficwa kwa mim ndio maana hukumu hii ikaitwa ikhfaa (kuficha). Inaitwa shafawi (simulizi) kwa vile mim hutamkwa kutoka kwenye midomo miwili (wa juu na wa chini). Pia katika lugha ya kiarabu mdomo pia hujulikana kama شَفَة 
Mifano
Suratul fil (105:4): ikhfaa shafawi ipo baina ya maneno tarmiihim na bihijaaratin.
تَرْمِيهِم بِحِجَارَةٍ مِّن سِجِّيلٍ
Suratul ‘Adiyaat (100:11): Ikhfaa shafawi ipo baina ya neno bihim rabbahum na bihim
إِنَّ رَبَّهُم بِهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّخَبِيرٌ
Suratul Ghaashiyah (88:22): Ikhfaa shawawi inapatikana baina ya ‘alayhim na bimuswaytir
لَّسْتَ عَلَيْهِم بِمُصَيْطِرٍ