Baadhi ya Du'aa za Kumuombea aliyetangulia mbele ya haki

Du’aa katika Qur’aan na Sunnah ambazo mtoto anaweza kumuomba mzazi wake aliyetangulia mbele ya haki pamoja na kuwaombea maiti wengine waislamu:

رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ الْحِسَاب  

Rabbana-ghfir liy waliwaalidayya walil Mu-uminiyna yawma yaquumul hisaab.

“Mola wetu! Unighufirie mimi na wazazi wangu wote wawili, na Waumini, siku ya kusimama hisabu” (Ibraahiym: 41) 
رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا
Rabbir-hamhumaa kamaa rabbayaaniy swaghiyraa.

“Mola wangu! Warehemu kama walivyonilea utotoni.  (Al-Israa: 24)

رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالإِيمَانِ وَلاَ تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَؤُوفٌ رَّحِيمٌ  

Rabbanaghfir lanaa wa liikhwaaninal-ladhiyna sabaquunaa bil Iymaani wa laa Taj’al fiy quluubinaa ghillal-lilladhiyna aamanuu Rabbannaa Innaka Rauufur-Rahiym.
“Mola wetu! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa Iymaan, wala Usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walioamini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu. (Al-Hashr: 10)
 رَبِّ اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ  
Rabbighfir liy waliwaalidayya  
“Mola wangu Mlezi! Nighufirie mimi na wazazi wangu.”  (Nuuh: 28)

 اَللَّهُمَّ اغْفِرْ لِلْمُؤمِنِينَ وَاْلمُؤمِنات وَالْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمات اَلأَحْيَاءِ مِنْهُمْ وَالأَمْوَات
Allaahumma-Ghfir lil-Muuminiyna wal-Muuminaat wal-Muslimiyna wal-Muslimaat, al-ahyaai minhum wal-amwaat
Ewe Mwenyezi Mungu Waghufurie Waumini wanaume na Waumini wanawake, Na Waislamu Wanaume na Waislamu wanawake, Waliohai miongoni mwao na waliokufa.

Du’aa iliyothibiti katika Sunnah ya kumuombea maiti katika sala ya maiti au wakati wowote mwingine

اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُ وَارْحَمْـه ، وَعافِهِ وَاعْفُ عَنْـه ، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـه ، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَه ، وَاغْسِلْـهُ بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ ، وَنَقِّـهِ مِنَ الْخطـايا كَما نَـقّيْتَ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ ، وَأَبْـدِلْهُ داراً خَـيْراً مِنْ دارِه ، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـه ، وَزَوْجَـاً خَـيْراً مِنْ زَوْجِه،  وَأَدْخِـلْهُ الْجَـنَّة ، وَأَعِـذْهُ مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار

Allaahumma-Ghfir-lahu war-ham-huu, wa 'Aafihi wa'afu 'anhu, wakrim nuzulahu, wa-Wassi' mudkhalahu, wa-Ghsil-hu bil-maai wath-thalji wal-Barad, wa Naqqihi minal-khatwaaya kamaa Naqqayta-th-thawabal-abyadhw Minad-danas, wa-Abdil-hu daaran khayran min daarihi, wa ahlan khayran min ahlihi, wa zawjan khayran min zawjihi, wa-Adkhil-huul-Jannata, wa A'idh-hu min 'adhaabil-Qabr wa 'adhaabin-Naar
“Ee Mwenyezi Mungu Msamehe na Umrehemu na Umuafu na Msamehe na Mtukuze kushuka kwake (kaburini) na Upanue kuingia kwake, na Muoshe na maji na kwa theluji na barafu na Mtakase na makosa kama Unavyoitakasa nguo nyeupe kutokana na uchafu, na Mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba yake, na jamaa bora kuliko jamaa zake, na mke bora kuliko mke wake, na Muingize Peponi na Mkinge na adhabu ya kaburi (na adhabu ya moto).