MASHARTI YA LAA ILAHA ILLA LLAAH

1. KUJUA MAANA YAKE:
Yatakiwa mtamkaji ajuwe maana ya neno hili na yale   matakwa yake, ikiwa ni kupinga uungu kwa asiye kuwa Allaah (سُبْحَنَه وَتَعْل) mmoja na kuuthibitisha kwake yeye peke yake.
كما قال تعالي(فَاعْلَمْ أَنَّهُ لاَ إِلَـهَ إِلأ اللَّه)
سورة محمد:19
Kama alivyo tueleza Allaah ndani ya kitabu chake kitukufu (Basi jua ya kwamba hapana Mungu ila Allaah(Mwenyezi Mungu mmoja)
Suurat Muhamad :19
Mmoja wetu anaweza kudhani kwamba kuifahamu ni kitu kidogo sana, na kwamba ni kitu cha moja kwa moja kwa kila Muislam kuijua, kiukweli ni kwamba wako ambao hutamka Laa ilaha illa Llaah kila siku na mara kwa mara wanafanya mambo ambayo ni ya kumshirikisha Allaah (سُبْحَنَه وَتَعْل). Wengi humshirikisha kwa kukosa kujua maana hasa ya Laa ilaha illa Llaah.
2. KUWA NA YAKINI JUU YA NENO HILI
Yatakiwa msemaji asiwe na shaka kabisa juu ya neno hili na matakwa yake. Kiasi kwamba yatakiwa ijengeke katika moyo wako ya kwamba Allaah (عز وجل) (Mwenyezi Mungu) wa kweli ni mmoja tu. Naye ndiye anayestahiki kuabudiwa na viumbe wote. Naye ndiye Muumbaji wa ulimwengu huu na vilivyomo. Naye ndiye mwenye Kuuhisha (kutoa uhai) na Kufisha. Naye ndiye Muendeshaji wa ulimwengu huu. Naye juu ya kila jambo ni Mjuzi. Naye juu ya kila jambo ni Muweza. Naye ndiye mwenye Kugawa riziki kwa waja wake....na kadhalika.
قال الله تعالي(إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آَمَنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنْفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ أُولَئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ )
الحجرات:15
Anasema Allaah (عز وجل) katika Qur ani (Hakika Waumini ni wale walio muamini Allaah na Mtume wake tena wasitie shaka kabisa, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao. Hao ndio wakweli.)Suurat Al Hujuraat:15
وَقَالَ صَلَّيْ الْلَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ(أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا الْلَّهُ وَأَنِّيَ رَسُوْلُ الْلَّهِ لَا يَلْقَىَ الْلَّهَ بِهِمَا عَبْدٌ غَيْرَ شَاكٍّ فِيْهِمَا إِلَّا دَخَلَ الْجَنَّةَ)
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Na anasema Mtume Muhammad (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) (Ninashuhudia ya kwamba hapana mola apaswaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah (Mwenyezi Mungu mmoja tu) na Mimi ni Mtume wa Allaah. Mja hawezi kukutana na Allaah akiwa na maneno haya pasina ya shaka (akiwa hana shaka juu ya maneno haya) isipokuwa Allaah atamuingiza peponi)
3. KUKUBALI MATAKWA YAKE KWA MOYO NA ULIMI
Yaani  kukubali kunakopingana na kukataa (kurudisha) na kutakabbari (kufanya kiburi) juu ya neno hili LAA ILLAAHA ILLAH LLAAH na matakwa yake. Kwani Allaah katueleza kuhusiana na watu watakao kuwa wakiadhibiwa motoni, na miongoni mwa sababu za kuadhibiwa kwao ni kupinga neno hili na matakwa yake.
قال الله تعالي(إِنَّا كَذَلِكَ نَفْعَلُ بِالْمُجْرِمِينَ .إِنَّهُمْ كَانُوا إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ يَسْتَكْبِرُونَ)     سورة  الصافات:34-35 
Anasema Mwenyezi Mungu  katika kitabu chake kitukufu(Hivyo ndivyo tutakavyowafanyia wakosefu.  Wao walipo kuwa wakiambiwa La ilaha illa 'Llahu Hapana mungu ila AllaaAllaah (عز وجل)h tu, wakijivuna. )
Suurat As swaaffaat 34-35
4. KUFUATA YALE AMBAYO LIMEJULISHA NENO HILI
Kwa maana ya kwamba yatakiwa mja awe ni mwenye kuyatekeleza yale aliyoamrishwa na Allaah na mwenye kujiweka mbali na yale aliyo katazwa.
قال الله تعالي في محكم التنزيل(وَمَنْ يُسْلِمْ وَجْهَهُ إِلَى اللَّهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَى وَإِلَى اللَّهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ )سورة لقمان:22
Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya kitabu chake kitukufu(Na mwenye kuuelekeza uso wake kwa Allaah, naye akawa anafanya wema, basi huyo hakika amekwisha kamata fundo lilio madhubuti. Na mwisho wa mambo yote ni kwa Allaah) Suurat Luqmaan:22
5. UKWELI:
Yatakiwa mtamkaji wa neno hili alitamke hali ya kuwa ni mwenye kusadikisha  katika moyo wake. Ulimi wake utamke kile anacho kiitakidi ndani ya moyo wake. Ulimi uwafikiane na moyo.
قال الله تعالي(وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يَقُولُ آَمَنَّا بِاللَّهِ وَبِالْيَوْمِ الْآَخِرِ وَمَا هُمْ بِمُؤْمِنِينَ . يُخَادِعُونَ اللَّهَ وَالَّذِينَ آَمَنُوا وَمَا يَخْدَعُونَ إِلَّا أَنْفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ)
البقرة:8-9
Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya Qur ani
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّهِ وَبِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ [٢:٨]يُخَادِعُونَ اللَّهَ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَمَا يَخْدَعُونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ [٢:٩]
(Na katika watu, wako wasemao: Tumemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, wala wao si wenye kuamini.   Wanatafuta kumdanganya Mwenyezi Mungu na wale walio amini, lakini hawadanganyi ila nafsi zao; nao hawatambui)Suurat:Al baqara:8-9
Watu hawa wanatamka tofauti na yale yaliyomo ndani ya nyoyo zao. Wanasema wao wamemuamini Allaah na siku ya mwisho (siku ya malipo) hali ya kuwa ukweli wa mambo hawaamini vitu hivyo. Wanamfanyia ujanja Allaah (عز وجل) na waumini, hali ya kuwa ukweli wa mambo ni kwamba wanajifanyia ujanja nafsi zao na hawalihisi hilo. Kwani ujanya waufanyao wa kudhihirisha kinyume na yale wanayo itakidi ndani ya nyoyo zao, uhakika wa madhara hautomrudia yoyote zaidi ya nafsi zao.

6. IKHLAAS
Ikhlaas maana yake ni: Mja kufanya jambo la utiifu kwa nia ya kutaka radhi za Allaah na makazi mema kesho akhera.
قال الله تعالي(وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ وَذَلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ )البينة:5
Anasema Allaah ndani ya Qur’ani tukufu (Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Allaah kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti)
 قال رسول الله صلي الله عليه وسل:(إن الله لا يقبل من العمل إلا ما كان له خالصاً وابتغي به وجهه )رواء أبو داوود
Kasema mtume Muhamad rehema na amani ziwe juu yake(Hakika Allaah hakubali matendo ya waja isipokuwa yale ambayo wameyafanya kwa ajili yake na kutaka radhi zake)
Kwa hiyo mtamkaji wa neno hili inakubidi ulitamke kwa kutaka radhi za Allaah. Si kulitamka kwa ajili ya kuwaridhisha watu, kwa ajili ya kuonekana fulani ni muislamu, kwa ajili ya maslahi fulani ya kidunia. Bali ulitamka kwa ajili ya  kutaka radhi za Allaah.

7. KULIPENDA NENO HILI
Yatakiwa msemaji ulipende neno hili na uwapende wale wenye kulitamka na kufuata wa masharti  ya neno hili. Vile vile yatakiwa kuchukia na kujiweka mbali na kila kile chenye kupelekea kushusha hadhi ya  neno hili au kutengua  sharti  miongoni mwa  masharti yake.

قال الله تعالي(وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يَتَّخِذُ مِنْ دُونِ اللَّهِ أَنْدَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّهِ وَالَّذِينَ آَمَنُوا أَشَدُّ حُبّ لِلَّهِ )البقرة:165

Anasema Allaah Mtukufu ndani ya Qur ani (Na katika watu wapo wanaochukua waungu wasiokuwa Allaah. Wanawapenda kama anavyopendwa Allaah. Lakini walio amini wanampenda Allaah zaidi sana)
Suurat: Al baqara:165
Katika sifa za waumini ni kumpanda Allaah (عز وجل). Kwani yeye peke yake ndiye aliye waumba naye ndiye anaye waruzuku, kuwaponya  na kwake yeye ndio marejeo ya viumbe wote.
Mpaka hapa tushajua maana ya LAA ILAHA ILLA LLAAH na masharti yake saba, masharti ambayo kwa kuyatekeleza masharti hayo basi neno hili litaku ni hoja ya mja mbele ya Allaah  na kumnufaisha msemaji wake. 
Makala ijayo inshaallaah tutazungumzia shahada ya pili ambayo ni Muhammad rasuulu llaah.