Al Idh-haar (آلإِظهَار)

Maana ya Idh haar
Idh haar katika lugha maana yake ni kudhihirisha au kuweka bayana yaani kuweka wazi, katika istilaah (kitaaluma) Idh haar maana yake ni kutamka herufi za idh-haar kwa ubainisho au udhihirisho wa wazi, kutoka kwenye sehemu yake ya matamshi na bila ya kutia ghunna.
Herufi za Idh haar
Herufi za idh haar ambazo ni sita
الهَمزَة وَالهَاء، وَالعَينُ وَالحَاءُ، وَالغَينُ وَالخَاءُ (ا، ه، ع، ح، غ، خ)
Hefuri za idh haar pia hujulikana kama herufi za kwenye koo (لحُرُوفُ الحَلقِيَّة) kwa sababu herufi hizi hutamkwa kutoka kwenye koo.
Namna idh haar inavyotokea
Idh haar hutokea iwapo nun saakina au herufi yenye tanwin itafuatiwa na moja kati ya herufi sita za kooni, mfuatano huu hutokea ama katika neno moja, kwa mfano (مِنْهَا) au baina ya maneno mawili kwa mfano (مِنْ أَيِّ شَيْءٍ خَلَقَهُ)
Namna ya kutamka idh haar
Kama ilivyoelezwa katika maana ya Idh haar herufi ya Idh haar hutamkwa kwa ubainisho (kudhihirishwa), kutoka katika sehemu yake ya kutamkia na bila ya kutia ghunna.
Mifano ya Idh haar
Suratil ‘Abasa, aya ya 18: Idh haar ni katika makutano ya nun saakina na alif hamza, baina ya maneno min ayyi, vile vile idh haar inapatikana baina ya makutano ya hamza yenye kisratain na khaa baina ya maneno shay-in na khalaqah.
مِنْ أَيِّ شَيْءٍ خَلَقَهُ
Suratil Fat ha, aya ya 7: Idh haar ipo katika makutano ya nun saakina na ‘ayn, katika neno an’amta.
صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ
Suratil Quraysh, aya ya 4: Idh haar ianapatikana katika makutano ya nun saakina na khaa, katika makutano ya maneno min na khawf.
الَّذِي أَطْعَمَهُمْ مِنْ جُوعٍ وَآمَنَهُمْ مِنْ خَوْفٍ
Suratil Fiyl, aya ya 3: Idh haar inapatikana katika maktano ya raa yenye fat ha tain baina ya maneno twayran na abaabiyl.
وَأَرْسَلَ عَلَيْهِمْ طَيْرًا أَبَابِيل َ
Suratut Takaathur, aya ya 8: Idh haar inapatikana baina ya makutano ya dhal kisra tain na ‘ayn baina ya maneno yawmaidhin na ‘ani