Tajwid

TAHADHARI
Somo la tajwid husomwa kwa msaada wa mwalimu mwenye ujuzi wa elimu hii. Japokuwa mwanafunzi anaweza kusoma hukmu za tajwid mwenyewe, inahitaji mjuzi wa elimu hii kuweza kujifunza kusoma Qur’an tukufu. Tunamshauri yoyote mwenye kutaka kujifunza somo hili kutafuta mwenye ujuzi wa kusoma kwa tajwid ili apate kujifunza kwa usahihi.
Kwa nyongeza mwanafunzi anaweza kutumia MP3, DVD au CD za wasomaji mbali mbali ili kuweza kujifunza kwa umahiri zaidi. Tunamuomba Allah atupe wepesi katika kujifunza na atujaalie elimu yenye manufaa, Amin.