Mawaidha


 

Shukrani zote zinamstahiki Allah, Mola mlezi wa viumbe wote. Rehma na amani zimshukie Mtume na watu wake, na masahaba wake pamoja na wote wenye kufuata mwenendo wake mpaka siku ya qiyama. 

Kuiamrisha familia kusali ni amri ya Allaah, amri hii imewekwa wazi bilaya utata wa aina yoyote kwenye Qur’aan, Allah ta’ala anatumbia katika Surat at Ta-Ha: 
وَأْمُرْ أَهْلَكَ بِٱلصَّلَوةِ وَٱصْطَبِرْ عَلَيْهَا ۖ لَا نَسْـَٔلُكَ رِزْقًا ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُكَ ۗ وَٱلْعَـقِبَةُ لِلتَّقْوَى ﴿٢٠:١٣٢﴾

Na waamrishe familia wako kusali, na uendelee mwenyewe kwa hayo. Sisi hatukuombi wewe riziki, bali Sisi ndio tunakuruzuku. Na mwisho mwema ni kwa mchamngu. (20:132)

YAA UKHTA HAARUN!



(يَا أُخْتَ هَارُونَ - EWE DADA YAKE HAARUN)  QUR’AAN 19:28
UTANGULIZI
Shukrani zote zinamsatahiki Mwenyezi Mungu Mola mlezi wa viumbe wote, Rehma na amani zimshukie Mtume Muhammad na ali zake na Sahaba zake pamoja na wote wenye kufuata mwenendo wake mpaka siku ya mwisho.
Wenye kuipinga Qur’aan hutoa madai kuhusu aya hii kwamba: Qur'aan inamwita Maryam Ukhta Haarun (Dada yake Haarun) wakati watu wawili hawa hawakuishi wakati mmoja, yaani wamepishana miaka kama 2000? Kwa hiyo Qur’aan imefanya kosa la Kihistoria.

Lengo la makala hii ni kuthibitisha kuwa Qur’an hapa haikufanya kosa bali wenye madai haya ama hufanya makusudi au hawakuelewa aya.
UFAFANUZI
Mwenyezi Mungu anatuambia katika Qur’aan tukufu aya ya 19:28 ninanukuu


يَا أُخْتَ هَارُونَ مَا كَانَ أَبُوكِ امْرَأَ سَوْءٍ وَمَا كَانَتْ أُمُّكِ بَغِيًّا 
Ewe dada yake Haarun! Baba yako hakuwa mtu muovu, wala mama yako hakuwa kahaba.

MWAKA MPYA WA KIISLAMU(1433)


Tarehe 26/11/11 ni siku inayoafikiana na  tarehe moja  ya mwezi Muharram, yaani mwezi wa kwanza wa kiislamu, kwa hiyo tumeingia mwaka mpya wa kiislamu.Tumetoka katika Mwaka wa 1432 na tumeingia 1433.
Idadi ya miaka hii ni tokea kuhama kwa mtume kutoka Makka na kuelekea Madina. Bila shaka kuna mazingatio makubwa sana juu ya kuhama Huku kwa mtume, mazingatio ambayo tutayazungumzia InshaaAllah.
Waislamu hatuna sherehe maalumu ndani ya siku hii inayo tambulika kisheria tokea enzi za mtume, masahaba zake na mpaka hivi sasa. Bali siku hii huadhimishwa kwa kukumbuka kipindi hiki ambayo baada yake uislamu ulipata dola ya kujitegemea na waislamu kuwa na uhuru wa kufanya watakavyo tofauti  na kipindi walichokuwa Makkah. Yaani dola ya Uislamu wa umma huu wa Mtume Muhammad ilianza tarehe 1/1/1 Hijria baada ya Waislamu kuhamia Madinah.

MAZINGATIO KATIKA HIJRAH


Bila shaka wengi wetu tumesoma au kusikia kuhusiana na Hijra(kuhama) ya mtume kutoka Makka na kuelekea Madina. Hapa ndipo ilipo anza tarehe ya kiislamu. Katika safari hii ya mtume kuna mazingatio mengi sana, leo hii tutazungumzia baadhi ya haya mazingatio:

1: Mazingatio ya uhamaji:
Mwenyezi Mungu alitoa idhini kwa Mtume wake na  Waumini kuhama toka Makkah kutokana na madhara mbali mbali waliyo kuwa wakiyapata kutoka kwa makafiri wa Kiquraysh. Katika haya madhara ilikuwa ni kuwazuia waislamu kuisimamisha dini yao, wakateswa na kuadhibiwa vikali.