Maana ya idghaam
Idghaam katika lugha maana yake ni kuingiza kitu kimoja katika chingine. Katika istilaah, idghaam maana yake ni kuunganisha herufi mbili, moja ikiwa ni yenye saakin na nyingine ina harakah. Misistizo wa matamshi unakuwa kwenye herufi yenye harakah ambayo ni ya pili na hivyo hefuri ya mwanzo huingizwa kwenye ya pili.
Hefuri za idghaam
Herufi za idghaam ni sita, nazo ni: ي، ر، م، ل، و، ن. Herufi hizi hujumuishwa kwa pamoja katika neno يَرمَلُونَ, neno hili hurahisisha kuzikumbuka herufi hizi.
Mgawanyiko wa idghaam
Idghaam imegawika makundi mawili nayo ni:
- Idghaam yenye ghunna (إِدغَام بِغُنَّة)
- Idghaam isiyo na ghunna (إِدغَام بِغَيرِ غُنَّة)
Herufi za Idghaam Yenye Ghunna: Idghaam yenye ghunna ina hefuri nne Kati ya sita za idghaam, herufi hizo ni ي، ن، م، و Herufi hizi kwa mjumuiko zinafanya neno يَنمُوَ, ambalo pia hurahisisha kuzikumbuka.
Matokeo ya Idghaam Yenye Ghunna: Idghaam yenye ghunna hutokea iwapo herufi moja kati ya herufi nne za idghaam yenye ghunna itatanguliwa na nun saakina au herufi yenye tanwin. Idghaam hutokea tu iwapo makutano haya ni baina ya maneno mawili.
Namna ya kutamka idghaam yenye ghunna: Sauti ya nun haitamkwi sawa sawa badala yake huingia kwenye herufi ya idghaam yenye ghunna yaani moja kati ya ي، ن، م، و na pia hutamkwa kwa ghunna ambayo ni sauti yenye kupitia kwenye mizizi ya pua.
Mifano ya Idghaam Yenye Ghunna.
لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْواً وَلَا كِذَّاباً
Idghaam yenye ghunna ipo baina ya neno min na maa-a
أَلَمْ نَخْلُقكُّم مِّن مَّاء مَّهِينٍ
Idghaam yenye ghunna ipo baina ya neno lahabin na watab
تَبَّتْ يَدَا أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ
Idghaam yenye ghunna ipo baina ya neno nafsin na wamaa
وَنَفْسٍ وَمَا سَوَّاهَا
Idghaam yenye ghunna ipo baina ya neno ywamaidhin na yasduru
يَوْمَئِذٍ يَصْدُرُ النَّاسُ أَشْتَاتاً لِّيُرَوْا أَعْمَالَهُمْ
Idghaam yenye ghunna ipo baina ya neno faman na ya’mal
فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْراً يَرَهُ