Idh haar Mutlaq (اِظحَار مُطلَق)

Idh haar mutlaq imekuwepo kutokana na kwamba idghaam yenye ghunna haitokei kwenye neno moja pekee. Ni lazima itokee katika makutano ya maneno mawili. Maneno yafuatayo kwenye Qur'ani tukufu hayana idghaam yenye ghunna ingawa kuna makutano ya nun saakina na herufi za idghaam yenye ghunna:-

1. Qinwaan (قِنوَانٌ)

    2. Swinwaan (صِنوَانٌ)

      3. Bun-yaan (بُنيَانً)

        4. Ad Dun-yaa (الدُّنيَا)
          Hivyo hukumu ya maneno haya ni Idh haar Mutlaq. Nun saakina (نْ) hutamkwa kwa kudhihirishwa na bil aya kutia ghunna.
          Mifano katika maandishi ya rangi nyekundu
          Suratil Kahfi, aya ya 21
          وَكَذَٰلِكَ أَعْثَرْنَا عَلَيْهِمْ لِيَعْلَمُوا أَنَّ وَعْدَ اللَّهِ حَقٌّ وَأَنَّ السَّاعَةَ لَا رَيْبَ فِيهَا إِذْ يَتَنَازَعُونَ بَيْنَهُمْ أَمْرَهُمْ ۖ فَقَالُوا ابْنُوا عَلَيْهِمْ بُنْيَانًا ۖ رَبُّهُمْ أَعْلَمُ بِهِمْ ۚ قَالَ الَّذِينَ غَلَبُوا عَلَىٰ أَمْرِهِمْ لَنَتَّخِذَنَّ عَلَيْهِمْ مَسْجِدًا
          Suratur Ra'd, aya ya 4:
          وَفِي الْأَرْضِ قِطَعٌ مُتَجَاوِرَاتٌ وَجَنَّاتٌ مِنْ أَعْنَابٍ وَزَرْعٌ وَنَخِيلٌ صِنْوَانٌ وَغَيْرُ صِنْوَانٍ يُسْقَىٰ بِمَاءٍ وَاحِدٍ وَنُفَضِّلُ بَعْضَهَا عَلَىٰ بَعْضٍ فِي الْأُكُلِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يَعْقِلُونَ

          Suratus Swaaf, aya ya 4:
          إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِهِ صَفًّا كَأَنَّهُمْ بُنْيَانٌ مَرْصُوصٌ
          Suratil A'la, aya ya 16:
          بَلْ تُؤْثِرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا
          Maneno haya yote hudhihirishwa kwa kutamkwa kutoka kwenye sehemu zake za matamshi na kutamkwa bila ya ghunna. Hukumu hii hujulikana kama Idh haar mutlaq (اِظحَار مُطلَق) Kutokea kwake ni makutano ya nun saakin na herufi za idh-haar yenye ghunna (يَنمُوَ) na nun saakina katika neno moja.

          Pia aya zifuatazo haziwi na idghaam yenye ghunna katika kusoma:
          يس وَالْقُرْآنِ الْحَكِيمِ
          ن ۚ وَالْقَلَمِ وَمَا يَسْطُرُونَ
          Zinaposomwa aya hizi msomaji hana budi kusimama baina ya (ن) nun na herufi ya idghaam yenye ghunna kwenye aya ya mwanzo baina ya sin na walqur'aan na kwenye aya ya pili baina ya nuun na walqalam