KIMBUNGA CHA SANDY NA MTAZAMO WA KIISLAMU

Kimbunga cha Sandy kinatarajiwa kutua katika Ardhi ya Mashariki ya Marekani likiwemo jiji la New York wakati wowote kuanzia hivi sasa, kimbunga hicho kinawafanya watu karibu milioni 50 waishi katika hali ya wasi wasi mno, kwetu sisi Waislamu matukio kama haya yana ibra, hutukumbusha kawmu kama vile za ‘Aad na Thamud, hutukumbusha watu mbali mbali ambao baada ya kufuru na uovu, Allaah aliwapelekea adhabu, inatukumbusha As-hab ul Ayka, As-habu al Hijri, Kawmu Tubba, Fir’awn na watu wa Misri, Kawmu Lut na watu waliomkanusha Nabii Nuuh (‘alahyi salam) Kwa hakika Kimbunga  cha Sandy kina mafunzo makubwa kwetu. 

Habib al Mustafa (صلي الله عليه وسلم) siku moja aliona wingu likitanda Madina, wingu katika jangwa si hali ya kawaida kwa vile ni sehemu yenye uchache wa mvua kwa kiasi kikubwa. Hivyo Mtume (صلي الله عليه وسلم) uso ulimbadlika kiasi kwamba 'Aisha (رضي الله عنه) aliona wazi wazi jinsi uso wa Mtume (صلي الله عليه وسلم) ulivyojawa na khofu, 'Aisha (رضي الله عنه) akamuuliza Mtume juu ya jambo gani lililomtia khofu. Mtume akamjibu kuwa watu waliotangulia kabla yake waliona wingu baada ya ukame wa muda mrefu, wakalifurahia wakidhani ni dalili ya mvua, kumbe wingu lile lilikuwa na adhabu ya Allaah (عز وجل), Miongoni mwa watu hao ni As-hab al Ayka. 


Huo ndio ulikuwa ufahamu wa Mtume kwamba kile tunajodhani sie kuwa ni majanga tu huwa mara nyingine ni adhabu kutoka kwa Allaah (تعلي) na si majanga tu yanayokuja bila ya sababu. Hata masahaba waliurithi mtazamo huo kwani katika mji wa Madina palitokea tetemeko la ardhi, wakati huo Madinat ur Rasul ikiwa chini ya Khilafa iliyoongozwa na Amir al Muminiyn Umar ibn Al Khatwaab (رضي الله عنه), Uma, baada ya kutokea tetemeko jengine (after shock) aliwakusanywa watu na kuwaambia waache kumuasi Allaah (عز وجل) la sivyo iwapo litatokea tetemeko jengine basi yeye angeuhama mji wa Madina. Hivyo pia ulikuwa ni ufahamu wa Umar kwamba majanga kama vile kimbunga, tetemeko la ardhi na mafuriko huwa mara nyingine ni adhabu miongoni mwa adhabu za Allaah (تعلي) kutokana na maasi na maovu. 


Leo tunatarajia kuona kimbunga cha Sandy kikiingia katika ardhi ya Marekani, nchi ambayo sio tu inaongoza kwa maasi bali pia inaongoza katika vita dhidi ya Uislamu kwa mbinu na njia mbali mbali, kuanzia vita vya silaha mpaka vita vya nyoyo na akili, yaani vita vya propaganda. Marekani kama As-hab al Ayka wamekiona kimbunga cha Sandy kabla ya kuingia katika miji yao, tofauti yao ni kwamba wakati watu wa Ayka walidhani wingu lingewaletea mvua na kuwapooza na ukame na joto, Marekani wana matumaini tu Sandy haiitafanya uharibifu na upotevu wa maisha mkubwa. Allaah ndiye mjuzi litakalotokea huko.


AS-HAB ALA AYKA 

As-hab al Ayka waliishi katoka Mji wa Madyan ambapo leo ni sehemu ya Syria, baada ya kuwa ni watu wapotofu Allaah (تعلي) aliwapelekea Mtume Shu'ayb (صلي الله عليه وسلم), Allaah anatuhabarisha katika Qur'aan kuhusu As-hab al ayka:

وَإِن كَانَ أَصْحَـٰبُ ٱلْأَيْكَةِ لَظَـٰلِمِينَ


Na hakika watu wa Kichakani [As-hab ala ayka] walikuwa wenye kudhulumu. [15:78]

Baada ya kuwa ni wenye kudhulumu Allaah alimpeleka Shu'ayb na ujumbe mmoja mkubwa pamoja na makatazo ya dhulma zao, Allaah anasema:


وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا ۗ قَالَ يَـٰقَوْمِ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُۥ ۖ قَدْ جَآءَتْكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ ۖ فَأَوْفُوا۟ ٱلْكَيْلَ وَٱلْمِيزَانَ وَلَا تَبْخَسُوا۟ ٱلنَّاسَ أَشْيَآءَهُمْ وَلَا تُفْسِدُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَـٰحِهَا ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ 

Na kwa watu wa Madyan tulimtuma ndugu yao Shua'ib. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Allaah. Hamna mungu mwengine isipo kuwa Yeye. Imekwisha kufikieni hoja wazi kutoka kwa Mola Mlezi wenu. Basi timizeni sawasawa vipimo na mizani, wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye uharibifu katika nchi, baada ya kuwa imekwisha tengenea. Hivi ndivyo bora kwenu ikiwa nyinyi ni Waumini. (7: 85)

Hivyo Shu'ayb aliwaamrishwa watu wa Ayka Kumuadubu Allaah, na maovu yao kubwa walilokatazwa ni kuwacha kufanya dhulma ya kupunja katika mizani na katazo la pili kuacha kufanya uharibifu katika nchi.


Watu wa Madyan hawakumsikiliza Nabii Shu'ayb [عليه السلم].


Insha-Allaah itaendelea….