LAA ILAAHA ILLA LLAAH


(لَا إِلَه إِلَّا الله) LAA ILAAHA ILLA LLAAH; Haya ni maneno ya upwekeshaji ambayo nafasi yake katika uislamu ni sawa na nafasi ya kichwa katika mwili.Nayo ndio wajibu mkubwa alio tuwajibisha Allah (سُبْحَنَه وَتَعْل). Mtu haingii katika uislamu isipokuwa kwa maneno haya, ambayo huitwa shahada mbili.
Ni nini maana ya maneno haya?
1.MAANA YA LAA ILAAHA ILLA LLAAH
LAA ILAAHA ILLA LLAAH: Maana yake ni Hakuna muabudiwa anaye stahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah (Mwenyezi Mungu)mmoja tu.
Kwa hiyo neno hilo limeungana kutokana na nguzo mbili muhimu nazo ni:-
1. Kupinga uungu wa kweli kwa asiye kuwa Allaah (سُبْحَنَه وَتَعْل) mmoja.
2. Kuthibithisha Uungu wa kweli kwa Allaah (عز وجل) mmoja peke yake na wala si pamoja na miungu mingine.
Kuna aya na hadithi mbali mbali ambazo zinazungumzia umuhimu wa LAA ILAHA ILLA LLAAH. Anasema Allaah (عز وجل) katika surat Muhammad aya:19

فَاعْلَمْ أَنَّهُ لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ
Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Allaah(Mwenyezi Mungu) mmoja
Na pia imepokelewa katika hadithi ifuatayo:

مَا رَوَاه الْبُخَارِي وَمُسْلِم مِن حَدِيْث عَبْد الْلَّه بْن عُمَر رَضِي الْلَّه عَنْهُمَا قَال: قَال رَسُوْل الْلَّه صَلَّى الْلَّه عَلَيْه وَسَلَّم: بُنِيَ الْإِسْلَام عَلَى خَمْس، شَهَادَة أَن لَا إِلَه إِلَّا الْلَّه، وَأَن مُحَمَّدا رَسُوْل الْلَّه، وَإِقَام الصَّلَاة، وَإِيْتَاء الْزَّكَاة، وَالْحَج، وَصَوْم رَمَضَان 
Amepokea Imamu Bukhari na Imamu Muslimu kutoka kwa Ibni Omar radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao kasema:Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehma na amani za Allaah ziwe juu yake. "Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano.Kushuhudia ya kwamba hapana mola apaswaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah mmoja ,na kushuhudia ya kwamba Muhammad ni mtume wa Allaah. Kusimamisha swala.Kutoa zakah.Kuhiji na kufunga ramadhaani."

 وَمَا رَوَاهُ الْتِّرْمِذِيُّ: عَنْ الْنَّبِيِّ صَلَّىَ الْلَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قَالَ  (خَيْرَ مَا قُلْتُ أَنَا وَالْنَّبِيُّوْنَ مِنْ قَبْلِيَ: لَا إِلَهَ إِلَّا الْلَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيْكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَىَ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيْرٌ) 
Kapokea Imamu Tirmidhii kwa riwaya yake, kutoka kwa Mtume Muhammad (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) kasema: “bora ya maneno niliyo yasema mimi na mitume kabla yangu: (LAA ILAHA ILLA LLAAH) hapana mola apaswaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah (عز وجل) mmoja peke yake pasina ya mshirika, ufalme ni wake na shukurani ni zake, Naye juu ya kila jambo ni muweza)”
Mpaka hapa tushajua maana ya LAA ILAHA ILLA LLAAH, lakini kuna jambo muhimu hapana budi kuzindua nalo ni kwamba: neno hili halimfai mwenye kulitamka mbele ya Allaah (عز وجل) isipokuwa kwa masharti. Je masharti yake ni yapi? Inshaallaah katika moja ya makala zijazo tutazungumzia masharti yake.