Idghaam katika lugha maana yake ni kuingiza kitu kimoja katika chingine, katika istilaah, idghaam maana yake ni kuunganisha herufi mbili moja ikiwa ni yenye saakin na nyengine ina harakah. Misistizo wa matamshi unakuwa kwenye herufi yenye harakah ambayo ni ya pili na hivyo hefuri ya mwanzo huingizwa kwenye ya pili. Kwa hiyo katika idhghaam mim saakina (مْ) inaingia kwenye mim (م) ambayo ina haraka.
Heruri ya Idghaam ndogo: Herufi yake ni moja nayo ni mim (م)
Namna Inavyotokea: Hukmu hii hutokea pale mim saakina inapofuatiwa na mim yenye haraka katika neno moja au baina ya maneno mawili.
Matamshi ya Idghaam Mithlayn: Idghaam hii hutamkwa kwa kuingiza mim saakina kwenye mim yenye haraka. Herufi mbili hizi hutamkwa kwa pamoja kwa msisitizo wa shaddah na ghunna.
Hukmu hii pia hujulikana kama Idghaam mithlayni ma’a lghunnah (إِدْغَام مِثْلَين صَغِيْرًا مَعَ الغُنَّة) Inaitwa mithlayni kwa sababu yerufi zote mbili zinazoingiana ni mim (م) na inaitwa Idghaam ndogo (الإِدْغَام الصَّغِيْر) kwa sababu mim saakina inatangulia na kufuatiwa na mim yenye haraka.
Mifano ya Idghaam Mithlayn
Suratil Baqrah aya (1:1): Idghaam mithlayn inatokea baina ya lam na mim, kwa herufi ya lam inaishia “mmm” ambayo ni mim saakina.
الم
Suratil Quraysh, (104:4): Idghaam mithlayni zipo mbili, ya mwanzo ni baina ya maneno At’amahum na min, na ya pili ni baina ya maneno Aamanahum na min
الَّذِي أَطْعَمَهُم مِّن جُوعٍ وَآمَنَهُم مِّنْ خَوْفٍ
Suratul Qadr (97:4): Idghaam mithlayni ipo baina ya maneno rabbihim na min.
تَنَزَّلُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمْرٍ
Suratil Buruj (85:20): Idghaam ndogo ipo baina ya maneno waraihim na muhiit
وَاللَّهُ مِن وَرَائِهِم مُّحِيطٌ
Suratul Mutafifiyn (83:4): Idghaam ndogo ipo baina ya maneno Annahum na mab’uthuun
أَلَا يَظُنُّ أُولَٰئِكَ أَنَّهُم مَّبْعُوثُونَ
Suratul Mutafifiyn (83:14): Idghaam swaghiir ipo baina ya maneno Qulubihim na maakanu.
كَلَّا ۖ بَلْ ۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ