Masjid Abdullah Quilliam ndio msikiti wa kwanza nchini Uingereza. Miskiti huu ulikuwa jengo lililonunuliwa na William Henry Quilliam aliyesilimu nchini Morocco na kuitwa Abdullah akiwa na umri wa miaka 17. Pia Abdullah Quilliam alikuwa mwandishi wa kwanza wa jarida la Kiislamu Uingereza. Jarida hili lilijulikana kama "Mwezi Muandamo" (The Cresent). Jarida hili lilitafsiriwa katika lugha 13 tofauti ambapo lilipelekea Sheikh Abdullah Quilliam kupata umaarufu mkubwa katika Ulimwengu wa Kiislamu.
Historia fupi ya msikiti huu ni kwamba ulianzishwa mwishoni mwa karne ya 18 (mwaka 1889) katika mji wa Liverpool na kuwepo kwa jamii ya kwanza ya Kiislamu katika mji huo. Mwanzilishi wa jamii hiyo Sheikh Abdullah Quilliam mara kwa mara alimtembelea khalifah wa mwisho wa Kiislamu wa Khilafatul Uthmaaniya, Abdulhamid wa pili huko nchini uturuki, ambaye alikuwa ni rafiki wa Sheikh Abdullah Quilliam. Pia katika msikiti huo palikuwa na Chuo cha Kiislam kilichoongwa na Nasrullah Warren.
Katika moja ya safari zake kwenda Uturuki Abdullah Qulliam alikaa muda mrefu akisoma Uislamu, aliporudi Uingereza alikuta jamii aliyoisilimisha imeuhama mji wa Liverpool, bila ya shaka kutokana na madhila makubwa waliyotapata, Waislamu hao walihamia mji wa Working ulioko kusini mwa Uingereza, Abdullah Qulliam nae aliwafuata Waislamu wenzake katika mji huo.
Kufuatia kuhama kwa jamii hii ya Waislamu msikiti wa Abdullah Quilliam ulikufa na kubaki kuwa "gofu". Hivi karibuni Waislamu wa UK wameanzisha "Abdullah Quilliam Society" kwa lengo la kufufua msikiti huu na kuanzisha makumbusho ya kuenzi kazi alizozifanya Sheikh Abdullah Quilliam. Pia sehemu hii itafanywa kuwa ni kitivo cha elimu na mijadala ya kidini. Kitivo hicho kwa sasa kipo katika ujenzi na kitakapo kamilika kabisa kitakuwa kimegharimu zaidi ya paundi milioni mbili na nusu.
Idadi ya watu waliosilimishwa na Sheikh Abdullah inasadikiwa kufikia watu 600, ambapo Kitivo hicho kipya pia kanakusudia kufanya utafiti juu ya maisha ya Waislamu hao.
Sheikh Abdullah Quilliam pia alimsilimsha Abdulhalim Nodda, mjapani wa kwanza katika nyakati zetu kusilimu, Sheikh Nodda naye pia ameacha athari kubwa nzuri ya Uislamu huko Japan.
Allah amremehu Sheikh Abdullah Henry Quilliam aliyefariki akiwa na umri wa miaka 76, ambapo alikuwa ni muislamu wa kwanza kutangaza Uislamu wazi wazi nchini UK kwa karne za karibuni.