Lengo la Mitume ni kuondoa Twaghuut

Allah sub-hanahu wa ta’ala amesema katika Surat An Nahl:

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ ۖ 
Na kwa hakika tumepeleka kwa kila umma Mtume kwamba: Muabuduni Allah, na epukeni Twaghuut. (16:36)
Maneno Muhimu:
Mtume: Mtu ambaye amechaguliwa na Allah kuwapelekea ujumbe wa Allah umma fulani, Mtume hupewa muongozo wa sheria (kitabu) 
Twaghuut: Vitu vinavyoabudiwa ambavyo havistahiki, miungu ya uongo ambapo hujumuisha watu ambao wamejipa uungu.
Mwenye kufata twaaghut hupelekea kwenye udhalim na upotofu
Maelezo ya aya
Aya hii inadhihirisha kwamba sababu pekee ya kuletwa Mitume ni kuwaongoa watu katika kumuabudu Allah na kuwaepusha na twaghuut (Ibada za uongo na viabudiwa vya uongo) Hii ni kuanzia Nuh 'alayhi salam ambapo ndio ibada za kishirikina zilipoanza mpaka huu umma wetu wa sasa hivi wa Mtume Muhammad salla Llahu ‘alayhi wa sallam.
Mafunzo ya Aya hii
  • Mitume imekuja kuongoa umam zao na kuondoa au kuzuia twaghuut
  • Pamoja na kwamba Mitume ilikuwa na misisitizo tofauti kutokana na upotofu wa umma, Mitume yote ilikuja kufundisha Tawhid na kuondoa shirk.
  • Kwa kila umma ambao ulipelekewa Mtume kutakuwa hakuna udhuru katika siku wa malipo kwa wale waliokataa kumfuata baada ya kufikishiwa ujumbe.
  • Aya hii pia ina maelezo ya shahada ndani yake yaani kumuabudu Allah subhanahu wa ta’ala pekee na kuepuka shirki.