Shirk katika Ar Rubuubiya

Kwa jina la Allah, mwingi wa rehma, mwenye kurehemu. Shukrani zote zinamsatahiki Allah(‘azza wa jall), Mola mlezi pekee anayestahiki kuabudiwa, kwake yeye ni mamlaka na amri zote. Nashuhudia kwamba hapana Mole anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah. Na nashuhudia kwamba Muhammad (salla Llahu ‘alayhi wa sallam) ni mja wake na mtume wake.
Shirk katika rubuubiya inaweza kugawanywa katika makundi mawili: 
Shirk kwa kumpa Allah wenza.
Sehemu hii ya shirk imegawika sehemu mbili, zote ziwawapa viumbe mamlaka ya Allah kuwa viumbe hivyo ndivyo vilivyo umba badala ya Allah sub-hanahu wa taa’ala, nazo ni:-
  1. Kwanza ni kuamini kwamba Allah ‘azza wa jall ana mshirika katika kuumba. Ushirika huo unaweza kuwa ni mshirika wa Allah ta’ala ni sawa naye au anamkaribia kwa ufalme wake katika kuumba. Shirk hii hupatikana zaidi katika karibu dini zote zisitokuwa Uislamu. Kundi hili la washirikina mara nyingi hutokana na imani za dini ambazo si Uislamu, wafuasi wa dini za namna hii ambao huamini visivyokuwa Mungu ni mungu pamoja na Mola mlezi na hujulikana kama Politheists.
  2. Shirk katika rubuubiya  pia hujumuisha imani kwamba kuna kiumbe chingine au mwingine badala ya Allah sub-hanahu wa ta’ala aliyeumba badala ya Allah  ta’ala kati ya ardhi na mbingu na vilivyomo ndani yake na vilivyomo nje yake.
Shirk kwa kukanusha kuwepo kwa Allah
Vile vile shirk katika rubuuubiya ni pamoja na kuamini kwamba hakuna Mola muumba na maumbile au viumbe viamekuja kwa njia nyingine kama vile wanavyoamini wenye kuamini nadharia ya Mpasuko mkubwa (Big bang theory), kwamba mpasuko huo umetokea wenyewe na Allah ‘azza wa jall hahusiki kabisa na uumbaji wa mbingu na ardhi pamoja na vilivyomo baina yake.
Sehemu ya hii ya shirk hutokana na nadharia za kifalsafa zenye lengo la kujaribu kuthibitisha uongo ulio wazi kwamba hakuna Mola muumba. Kundi hili katika nchi za Kimagharibi limekuwa likipata wafuasi zaidi katika miaka ya karibuni, wafuasi wa imani hii ya kutokuwepo kwa Mungu hujulikana kama Atheists.
Ni vigumu kumkuta Muislamu anafanya shirk katika rubuubiya, hata hivyo wako wale waliochanganya falasafa na nadharia mbali mbali katika imani na itikadi zao, nao hutumbikia kwenye shirk hii. Mfano wake  ni nadharia ya mpasuko mkubwa (big bang theory) au nadharia ya Charles Darwin juu ya asili ya binadamu (theory of evolution).  Wengi wao hutumbukia katika imani za namna hii bila ya kujua kwamba kufanya hivyo kumewapelekea kwenye kuwa washirikina.