Hadith zimegawika sehemu mbili kuu. Nazo hi Isnaad na Matn.
Isnaad:
Isnaad ni msururu wa wasimuliaji au wapokeaji wa hadith. Hii hujumuisha majina ya wasimulizi kuanzia alyemsikia Mtume (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) ambaye ni sahaba na kufuatia wengine.
Mfano:
حَدَّثَنَا الْحُمَيْدِيُّ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ الزُّبَيْرِ قَالَ حَدَّثَنَا سُفْيَانُ قَالَ حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ الْأَنْصَارِيُّ قَالَ أَخْبَرَنِي مُحَمَّدُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ التَّيْمِيُّ أَنَّهُ سَمِعَ عَلْقَمَةَ بْنَ وَقَّاصٍ اللَّيْثِيَّ يَقُولُ سَمِعْتُ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَلَى الْمِنْبَرِ قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ
Majina haya hujipanga kuanzia wa mwisho kuja wa mwanzo, yaani wa mwisho anakuwa ni yule aliyemsikia Mtume (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ).
Mara nyingi katika uandikaji wa hadith katika vitabu ambavyo si vya somo la Hadith Matn hufupishwa na kuandikwa yule anayesimulia kutoka kwa Mtume Muhammad (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) mwenyewe. Baadhi ya mapokeaji maarufu ni pamoja na Abu Hurayra, Anas Bin Malik, Said Al Khudri na Aysha Bint AbuBakr (Allah awawie radhi)

Matn:
Matn ni hadith yenyewe, yaani ni maneno au matendo au maamuzi ya Mtume (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) au maelezo juu ya tabia au maumbile yake Mtume Muhammad (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)
Mfano:
إِنَّمَا الْأَعْمَالُ بِالنِّيَّاتِ وَإِنَّمَا لِكُلِّ امْرِئٍ مَا نَوَى فَمَنْ كَانَتْ هِجْرَتُهُ إِلَى دُنْيَا يُصِيبُهَا أَوْ إِلَى امْرَأَةٍ يَنْكِحُهَا فَهِجْرَتُهُ إِلَى مَا هَاجَرَ إِلَيْهِ